• HABARI MPYA

  Monday, May 28, 2018

  YONDAN AMALIZA ADHABU, AREJEA KIKOSINI YANGA MECHI YA MWISHO LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Yanga SC, Kevin Patrick Yondan ameruhusiwa kuendelea kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa kwa mechi nne kufuatia kumtemea mate beki wa Simba, Asante Kwasi.
  Yondan alimtemea mate beki Mghana wa Wekundu wa Msimbazi katika mechi dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba Aprili 29, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Yanga ikifungwa 1-0 na baada ya hapo akasimamishwa kwa muda hadi suala lake litakapotolewa ufafanuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
  Msemaji wa klabu ya Yanga, Dismass Ten ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wamepokea barua kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikisema Yondan yuko huru kucheza baada ya kumaliza adhabu yake.

  Kevin Yondan ameruhusiwa kuendelea kucheza Ligi Kuu baada ya kumaliza adhabu yake  

  “Tumwpokea barua ya TFF ikisema Yondan anaweza kuendelea kucheza baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa mechi nne,”amesema Ten. 
  Hata hivyo, hakuna kumbukumbu za taarifa za kufungiwa kwa Yondan, zaidi ya taarifa ya mwisho iliyosema mchezaji huyo hakutokea katika kikao cha Kamati ya Nidhamu.
  Kwa barua ya TFF, Yondan anaweza akaibukia kwenye kikosi cha Yanga kitakachomenyana na Azam FC katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa utakaoanza Saa 2:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YONDAN AMALIZA ADHABU, AREJEA KIKOSINI YANGA MECHI YA MWISHO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top