• HABARI MPYA

  Friday, May 25, 2018

  MAREFA WA LEO WALIVYOWAUDHI NA KUWASONONESHA WAPENZI WA YANGA MECHI NA RUVU

  Shabiki wa Yanga akipiga kelele kwa hisia na jazba kali dhidi ya marefa wa mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu yao na Ruvu Shooting FC ya Pwani uliomalizika kwa sare ya 2-2 Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa mjini Dar es Salaam
  Mashabiki wengine hawa wakiwaporomoshea maneno makali marefa 
  Na akina baba nao hawakuwa nyuma katika vita hiyo. Jamaa wa kulia naye kakunja ngumi
  Bwana mkubwa huyu na wanawawe aliishia kustaajabu tu 
  Akina mama hawa kama wamemwagiwa maji
  Mashabiki wengine wakiwashambulia kwa maneno marefa
  Kushoto kwa masikitiko makubwa amejifunika kanga na wa kulia akajifunika kofia asione maudhi ya refa, huku shoga yao katikati 'akirusha povu'
  Katikati mwanamama huyu akiwachamba marefa huku akinababa wakiangalia tu kwa hasira
  Ilikuwa huzuni leo kwa mashabiki wa Yanga leo uwanja wa Uhuru
  Lakini kwa mashabiki wachache wa mahasimu wao, Simba SC waliojitokeza uwanjani hapo ilikuwa furaha namna hii
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAREFA WA LEO WALIVYOWAUDHI NA KUWASONONESHA WAPENZI WA YANGA MECHI NA RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top