• HABARI MPYA

    Wednesday, May 09, 2018

    BODI YA LIGI YA TFF YAZITHIBITSHA ZILIZOPANDA LIGi KIUU MSIMU UJAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BODI ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezithibitisha timu za  JKT Tanzania, African Lyon, Manispaa ya Kinondoni (KMC) za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Biashara United FC ya Mara na Alliance Schools FC ya Mwanza kupanda daraja.
    Taarifa ya Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba msimu wa Ligi wa 2017/2018 kwa mujibu wa Kalenda ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) unamalizika Mei 31, 2018.
    Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambao ndiyo waendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) tunatoa pongezi kwa timu ambazo zimefanikiwa kupanda daraja.
    Kocha wa JKT Tanzania, Bakari Shine timu yake imethibitishwa kurejea Ligi Kuu

    Kwa upande wa FDL zilizopanda kwenda VPL msimu wa 2018/2019 kulingana na msimamo wa mwisho wa Ligi hiyo ni; Kundi A ni JKT Tanzania FC ya Dar es Salaam na African Lyon ya Dar es Salaam.
    Kundi B ni Kinondoni Municipal Council FC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga wakati Kundi C ni Biashara United FC ya Musoma na Alliance Schools FC ya Mwanza.
    Kwa upande wa SDL zilizopanda kwenda FDL msimu wa 2018/2019 ni timu nne zilizoongoza makundi pamoja na washindwa bora (best looser) watatu. Kundi A ni Reha FC ya Dar es Salaam, Kundi B ni Arusha FC ya Arusha, Green Warriors ya Dar es Salaam, na Mashujaa FC ya Kigoma.
    Washindwa bora ni Namungo FC ya Lindi,  Pepsi FC ya Dar es Salaam, na Boma FC ya Kyela, Mbeya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BODI YA LIGI YA TFF YAZITHIBITSHA ZILIZOPANDA LIGi KIUU MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top