• HABARI MPYA

  Tuesday, May 08, 2018

  AFRICAN LYON YALETA KOCHA MFARANSA, YAPANIA KUFANYA VYEMA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MMILIKI wa African Lyon, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ amesema kwamba wafadhili wamemsaidia kupata kocha Mfaransa mwenye leseni A ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Zamunda alisema yupo kwenye maandalizi ya Ligi Kuu na dhamira ni kuhakikisha African Lyon inafanya vyema kwenye Ligi Kuu msimu ujao.
  “Tunataka kufanya vizuri msimu ujao, tuwe timu ya ushindani tuonyeshe tofauti na misimu yote iliyotangulia. Na ili tufanikiwe, lazima tuwe na maandalizi mazuri,”alisema. 
  Zamunda amesema kwa sasa ana uzoefu wa miaka minane ya kuendesha timu ya mpira wa miguu nchini Tanzania ambao anataka autumie kuhakikisha Lyon inafanya vizuri msimu ujao.
  Rahim Kangenzi (kushoto), akiwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Roberto Di Matteo (kulia)

  African Lyon imekuwa ni timu yenye uzoefu wa kucheza na madaraja mawili, Ligi Kuu na Daraja la Kwanza tangu ipande kwa mara ya kwanza msimu wa 2009/2010.
  Ilipanda chini ya umiliki wa mfanyabiashara, Mohammed ‘Mo’ Dewji ambaye aliinunua kutoka kwa Jamal Kisongo na wafanyabiashara wa soko la Mbagala, ambaye naye akamuuzia Zamunda miaka miwili baadaye.
  Lyon ni kati ya timu sita zilizopanda Ligi Kuu msimu huu, nyingine ni KMC, JKT Tanzania za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Biashara United ya Mara na Alliance Schools ya Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AFRICAN LYON YALETA KOCHA MFARANSA, YAPANIA KUFANYA VYEMA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top