• HABARI MPYA

  Tuesday, May 08, 2018

  FERGUSON APATA NAFUU, AANZA KUZUNGUMZA NA WANAFAMILIA, MARAFIKI

  KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameanza kupata nafuu kufuatia kufanyiwa upasuaji wa ubongo wake ulioharibika.
  Kocha huyo mwenye mafanikio zaidi katika soka ya Uingereza anabaki kitengo cha wagonjwa walio chini ya uangalizi makini, lakini jana alikuwa anaweza kuketi na kuzungumza na wanafamilia yake na marafiki katika hospitali ya Salford Royal alikolazwa tangu Jumamosi.
  Upasuaji ulienda vizuri na kocha huyo mwenye umri wa miaka 76 amesema tiba zimempatia ahueni.
  Pamoja na hayo inaelezwa ataendelea kuimarika taratibu hadi kuwa timamu. 
  Sir Alex Ferguson ameanza kupata nafuu kufuatia kufanyiwa upasuaji wa ubongo wake ulioharibika

  Habari za kuugua kwa Ferguson zimeitikisa dunia, kutokana na namna Mscotland huyo alijijengea heshima kwenye ulimwengu wa soka akiipa timu hiyo mataji 38 katika miaka yake 26 ya kufanya kazi Old Trafford kabla ya kustaafu mwaka 2013.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FERGUSON APATA NAFUU, AANZA KUZUNGUMZA NA WANAFAMILIA, MARAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top