• HABARI MPYA

  Wednesday, May 09, 2018

  ABDI BANDA ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA APRILI AFRIKA KUSINI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Aprili wa klabu yake, Baroka FC ya Afrika Kusini.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online kwa simu kutoka Johannesburg, Afrika Kusini, Banda amesema kwamba anamshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo na anawashukuru Watanzania kwa kuendelea kumpa sapoti.
  “Kwanza kabisa ninapenda kumshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa nne, ukiangalia nipo katika msimiu wangu wa kwanza tu Baroka, lakini leo mchango wangu umeonekana na kupata bahati ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora,”amesema Banda na kuongeza;
  Abdi Banda akikabidhiwa tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Aprili wa Baroka FC  

  “Kuna wachezaji wengi kutoka nchi mbalimbali, kutoka Namibia na wengine wa hapa hapa, hii inaonyesha kuwa Watanzania tunaweza tukiamua na tunaendelea kuitangaza nchi yetu katika mataifa mbalimbali"amesema Banda
  Banda alijiunga na Klabu ya Baroka FC ya nchini Afrika kusini Julai 8, mwaka jana akitokea Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo nayo ilimtoa Coastal Union ya Tanga mwaka 2015.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ABDI BANDA ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA APRILI AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top