• HABARI MPYA

    Sunday, April 05, 2026

    NAMUNGO FC YAAMBULIA SARE KWA JKT TANZANIA, 2-2 RUANGWA


    TIMU ya Namungo FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
    Mabao ya Namungo FC yamefumgwa na kiungo Jacob Raymond Massawe dakika ya 25 na mshambuliaji Herbert Charles Lukindo dakika ya 63, wakati ya JKT Tanzania yamefungwa na washambuliaji, Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 66 na Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 90’+2.
    Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 18 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya nane, wakati JKT Tanzania inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 18 pia, ingawa inabaki nafasi ya nne.

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAMUNGO FC YAAMBULIA SARE KWA JKT TANZANIA, 2-2 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top