• HABARI MPYA

    Thursday, April 09, 2026

    SIMBA SC NAYO YAISHINDWA TRA UNITED ARUSHA, ZATOKA SULUHU

    TIMU ya Simba SC imetoa sare ya bila mabao na wenyeji, TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
    Kwa matokeo hayo, TRA inayofundishwa na Kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje inafikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba ikiizidi tu wastani wa mabao Dodoma Joni FC baada ya wote kucheza mechi 18.
    Kwa upande wao Simba SC wanafikisha pointi 36 katika mchezo wa 17, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi nane na mabingwa watetezi, Yanga ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC NAYO YAISHINDWA TRA UNITED ARUSHA, ZATOKA SULUHU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top