TIMU ya Mashujaa imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kwa matokeo hayo, Pamba Jiji FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Mkenya, Francis Barasa inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 17 ikisalia nafasi ya tano, wakati Mashujaa FC ya Kocha mzawa, Jamhuri Kihwelo inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 18 nayo ikisalia nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment