• HABARI MPYA

  Sunday, May 20, 2018

  NGORONGORO YAPIGWA 4-1 NA MALI BAMAKO…YATUPWA NJE MBIO ZA NIGER 2019

  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imetupwa pembeni ya mbio za kuwania tiketi za Fainali za U20 Afrika baada ya kuchapwa mabao 4-1 na wenyeji, Mali Uwanja wa Omnisports Modibo Keita mjini Bamako leo.
  Matokeo hayo yanamaanisha Tanzania inatolewa katika kinyang’aniyiro cha tiketi ya Niger mwakani kwa jumla ya mabao 6-2, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Mei 13 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mali sasa itakutana na mshindi wa jumla kati ya Cameroon na Uganda katika hatua ya mwisho ya mchujo kuelekea Niger 2019. 
  Benchi la Ufundi la Ngorongoro Heroes. Kushoto kocha mkuu, Ammy Ninje
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO YAPIGWA 4-1 NA MALI BAMAKO…YATUPWA NJE MBIO ZA NIGER 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top