• HABARI MPYA

  Sunday, May 20, 2018

  CHILUNDA APIGA HAT TRICK AZAM FC YAITANDIKA PRISONS 4-1 LIGI KUU CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DXAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Shaaban Iddi Chiliunda leo amefunga mabao matatu peke yake, timu yake Azam FC ikiibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi 55 baada ya kucheza mechi 29 na kuendelea kukamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya mabingwa, Simba SC wenye pointi 68 za mechi 29, wakati Prisons inabaki na pointi zake 45 katika nafasi ya nne. 

  Shaaban Iddi amefunga mabao matatu peke yake Azam FC ikiichapa Prisons 4-1 leo

  Chilunda alifunga mabao yote hayo kipindi cha kwanza huku kiungo Frank Raymond Domayo akifunga bao lingine kipindi hicho, kabla ya Mohammed Rashid kuifungia Tanzania Prisons la kufutia machozi kipindi cha pili.   
  Mechi nyigine ya Ligi Kuu jioni ya leo, bao pekee la kiungo Hassan Dilunga dakika ya 81 limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC Uwanja wa Saba Saba.
  Matokeo hayo yanazidi kuisogeza Daraja la Kwanza Njombe Mji FC ikibaki na pointi zake 22 baada ya kucheza mechi 29 na inaendelea kushika mkia kwenye Ligi Kuu ya timu 16 ambayo timu zake mbili zitashuka Daraja.
  Mtibwa Sugar inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 29 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya sita, nyuma ya Singida United pointi 44, Tanzania Prisons 45, Yanga 48, Azam FC 55 na Simba SC mabingwa wenye pointi 68. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHILUNDA APIGA HAT TRICK AZAM FC YAITANDIKA PRISONS 4-1 LIGI KUU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top