• HABARI MPYA

  Sunday, May 20, 2018

  AKINA SAMATTA WASHINDA UGENINI 2-1 UBELGIJI KUWANIA TIKETI YA ULAYA

  Na Mwandishi Wetu, ANDERLECHT
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza kwa dakika zote 90 leo timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Anderlecht katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
  Katika mchezo huo wa mchujo wa kuwania ya kucheza michuano ya Ulaya mwakani uliofanyika Uwanja wa Constant Vanden Stock mjini Brusells, Ubelgiji mabao ya Genk yalifungwa na Wabelgiji, beki Dries Wouters dakika ya 35 na mshambuliaji Leandro Trossard dakika ya 37.
  Bao la kufutia machozi la wenyeji, Anderlecht lilifungwa na mshambuliaji kutoka Poland, Lukasz Teodorczyk dakika ya 53 na kwa matokeo hayo, Genk ianamaliza nafasi ya tano kwenye msimamo na Jumapili ijayo watamenyana na ama  Lokeren au Zulte Waregem kuwania tiketi ya mwisho ya Ulaya.

  Mbwana Samatta (katikati) akishangilia na wenzake ushindi wa 2-1 dhidi ya Anderlecht leo  

  Samatta leo amecheza mechi yake ya 89 tangu Nahodha huyo wa Taifa Stars ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kati ya hizo akiwa amefunga mabao 25.
  Kikosi cha Anderlecht kilikuwa; M. Sels, O. Deschacht, A. Najar/ F. Amuzu dk46, U. Spajic, S. Kums, R. Morioka/ A. Lokonga dk84, K. Mbodji, A. Trebel, P. Gerkens, A. Saelemaekers na L. Teodorczyk.
  KRC Genk; D. Vukovic, B. Nastic, O. Colley, D. Wouters/ S. Berge dk64, J. Aidoo, Pozuelo/ S. Schrijvers dk79, I. Seck, Clinton Mata, L. Trossard, M. Samatta na D. N'Dongala/ T. Buffel dk85.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AKINA SAMATTA WASHINDA UGENINI 2-1 UBELGIJI KUWANIA TIKETI YA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top