• HABARI MPYA

  Monday, May 21, 2018

  MSUVA AFUNGA BAO PEKEE DIFAA HASSAN EL JADIDA YASHINDA MECHI YA MWISHO LIGI YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana limeipa ushindi wa 1-0 Difaa Hassan El Jadida katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco dhidi ya Olympic Safi.
  Msuva alifunga bao hilo dakika ya 43 katika mchezo huo wa ligi hiyo maarufu kama Botola Pro uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan.
  Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El Jadida inafikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 30 na kumaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Botola Pro nyuma ya FUS Rabat pointi 49, Hassania Agadir pointi 51 sawa na Wydad Casablanca, wakati Ittihad Tanger wenye pointi 52 ndiyo mabingwa.

  Simon Msuva ameipa ushindi wa 1-0 Difaa Hassan El Jadida katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Morocco jana

  Baada ya kumaliza mechi za Ligi, Msuva anarejea nyumbani kwa mapumziko ya kupisha Fainali za Kombe la Dunia na atarudi Morocco Julai kwa mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya 16 Bora.
  Baada ya sare ya 1-1 na MC Alger nchini Algeria na kufungwa 2-0 nyumbani na TP Mazembe, akina Msuva watakamilisha mechi zao za mzunguko wa kwanza wa kundi lao, B kwa kumenyana na ES Setif nchini Algeria Julai 17.
  Na ni hao hao Setif watakaoanza nao katika Raundi ya pili nyumbani Julai 27 kabla ya kurudiana pia na MC Alger Agosti 18 na kwenda kukamilisha hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa kwa kumenyana na TP Mazembe Julai 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AFUNGA BAO PEKEE DIFAA HASSAN EL JADIDA YASHINDA MECHI YA MWISHO LIGI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top