• HABARI MPYA

  Monday, May 21, 2018

  FREE STATE STARS WATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA KUSINI

  TIMU ya Free State Stars itaungana na Kaizer Chiefs kuiwakilisha Afrika Kusini katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
  Hiyo ni baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Maritzburg United, bao pekee la Goodman Dlamini dakika ya 37 katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA), maarufu kama Nedbank Uwanja wa Cape Town juzi jioni.
  Timu hizo zilifanya maajabu msimu huu kwa kuvitoa vigogo kama Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates hadi kukutana kwenye fainali.
  Hilo linakuwa taji la kwanza kwa timu hiyo ya zamani ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Ngassa tangu mwaka 1994.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FREE STATE STARS WATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top