• HABARI MPYA

  Friday, May 11, 2018

  YANGA WAIOMBA LIPULI IWAPE ADAM SALAMBA AWASAIDIE KWENYE MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa klabu ya Yanga SC umewasilisha maombi klabu ya Lipuli FC ya Iringa kumchukua kwa mkopo mshambuliaji, Adam Salamba imtumie katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
  Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa kwamba kwa sababu kanuni zinawaruhusu kuongeza wachezaji baada ya kuingia hatua ya makundi, wanataka kumsajili Salamba.
  “Tayari tumewaandikia barua Lipuli FC kumuomba Adam Salamba kwa ajili ya Kombe la Shirikisho Afrika,”amesema Mkwasa.
  Pamoja na Salamba, inafahamika Yanga SC pia inamtaka mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habib Kiyombo na
  Adam Salamba yuko mbioni kujiunga na Yanga SC kwa ajili ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika

  Mnigeria, Quadri Kola anayecheza Botswana.
  Yanga ilianza vibaya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 4-0 na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Kombe Jumapili Uwanja wa Julai 5, 1962.
  Na baada ya mechi keshokutwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Yanga itabaki kambini mjini humo kujiandaa kwa mchezo wa pili wa Kundi Kombe la Shirikisho Afrika Jumatano Uwanja wa Taifa,. Dar es Salaam.
  Baada ya mechi Rayon Sport katikati ya wiki ijayo, michuano ya Kombe la Shirikisho itasimama kupisha Fainali za kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi. Yanga watakamilisha mechi zao za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
  Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAIOMBA LIPULI IWAPE ADAM SALAMBA AWASAIDIE KWENYE MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top