• HABARI MPYA

  Wednesday, May 09, 2018

  SIMBA SC KUIFUATA SINGIDA UNITED KESHO KWENYE SHEREHE ZA UBINGWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Alhamisi kwenda Singida kwa ajili ya mchezo wake wa Jumapili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Singida United Uwanja wa Namfua.
  Simba SC inaupa uzito mchezo huo, kwa sababu ni ambao wanaweza kukabidhiwa Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu kama watashinda au kutoa sare.
  Lakini shangwe za ubingwa Simba SC zinaanza kuanza kesho jioni iwapo, mahasimu wao wakubwa, Yanga hawatashinda dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.  
  Yanga SC imepoteza nafasi ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu, kufuatia kufungwa 1-0 na mahasimu wao, Simba SC Aprili 29, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam bao pekee la Erasto Edward Nyoni.  
  Simba ina pointi 65 baada ya kucheza mechi 27 na Yanga yenye pointi 48 za mechi 24, inaweza kumaliza na pointi 66 ikishinda mechi zake zote zilizosalia- maana yake hata wakitoa sare na Tanzania Prisons kesho Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Wekundu wa Msimbazi watatawazwa kuwa wafalme wa Tanzania Bara.
  Simba imeweka kambi katoka hoteli ya Sea Scape, huku ikifanya mazoezi jirani na hapo katika Uwanja wa White Sands, eneo la Mbezi Beach mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUIFUATA SINGIDA UNITED KESHO KWENYE SHEREHE ZA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top