• HABARI MPYA

  Friday, May 11, 2018

  N'GOLO KANTE MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA CHELSEA TENA

  N'Golo Kante (katikati) akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  WASHINDI WA TUZO ZA CHELSEA 2017/18

  Mchezaji Bora wa Mwaka - N'Golo Kante
  Mchezaji Bora wa Wachezaji - Willian
  Mchezaji Bora Chipukizi- Andreas Christensen
  Bao Bora la Msimu - Willian ( v Brighton, Jan 18)
  Mchezaji Bora wa mwaka wa Chelsea ya Wanawake - Fran Kirby
  Mchezaji Bora wa Msimu wa Akademi - Reece James 
  KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa, N'Golo Kante ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Chelsea kwa mara ya pili mfululizo.
  Kiungo ameendelea kung'ara Chelsea ingawa haikuwa katika msimu mzuri akitwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo.
  Mchezaji mwenzake, Mbrazil Willian amefanikiwa kuchukua tuzo mbili usiku wa jana West Kensington, akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji na Bao Bora la Msimu.
  Usiku wa jana pia ilishuhudiwa wachezaji na viongozi wakijumuika pamoja kushangilia mafanikio ya msimiu.
  Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka imechukuliwa na Andreas Christensen, Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chelsea ya Wanawake ni Fran Kirby na Mchezaji Bora wa Msimu wa Akademi ni Reece James. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: N'GOLO KANTE MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA CHELSEA TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top