• HABARI MPYA

    Wednesday, May 09, 2018

    MWADINI ALI MCHEZAJI BORA WA MWEZI AZAM FC, AWABWANA SURE BOY NA DOMAYO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA Mwadini Ally, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Machi wa klabu yake, Azam FC.
    Mwadini ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwa na kiwango kizuri mwezi huo akicheza jumla ya mechi nne (sawa na dakika 360) akiruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu.
    Kipa huyo amevuna asilimia 52 za kura 1,000 zilizopigwa na mashabiki wa soka kwenye ukurasa wa mtandao wetu wa facebook, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amevuna asilimia 25 huku Frank Domayo ‘Chumvi’ naye akivuna asilimia 23 ya kura hizo.
    Hii ni mara ya kwanza kwa kipa huyo mzaliwa wa Unguja, visiwani Zanzibar kubeba tuzo hiyo, ambapo hadi hivi sasa wengine waliotwaa msimu huu ni Yakubu Mohammed, Mbaraka Yusuph, Himid Mao ‘Ninja’, Razak Abalora na Yahya Zayed.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWADINI ALI MCHEZAJI BORA WA MWEZI AZAM FC, AWABWANA SURE BOY NA DOMAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top