• HABARI MPYA

  Friday, May 18, 2018

  MBAO FC YAIPIGA 1-0 STAND UNITED KAMBARAGE, BADO POINTI TATU KUBAKI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la kiungo Mrundi, Yusuph Ndikumana dakika ya 19 kwa penalti limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Mbao FC dhidi ya wenyeji Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kwa ushindi huo, Mbao FC inafikisha pointi 30 katika mechi ya 28, ingawa inaendelea kukamata nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi na inahitaji kushonda mechi moja kati ya mbili zilizobaki ili kujihakikishia kuendelea kuwa mwanachama wa Ligi Kuu msimu ujao.
  Stand United yenyewe inabaki na pointi zake 32 baada ya kucheza mechi 29 na tayari ina uhakika wa kuendelea kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi mbili, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Simba SC wataikaribisha Kagera Sugar na Njombe Mji FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja Saba Saba mjini Njombe.
  Jumapili mbaki na Yanga SC kumenyana na Mwadui FC, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam, wenyeji Azam FC wataikaribisha Tanzania Prisons.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBAO FC YAIPIGA 1-0 STAND UNITED KAMBARAGE, BADO POINTI TATU KUBAKI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top