• HABARI MPYA

    Friday, May 18, 2018

    LACAZETTE NA MARTIAL WOTE NJE KIKOSI CHA UFARANSA KOMBE LA DUNIA

    WASHAMBULIAJI wanaocheza Ligi Kuu ya England, Anthony Martial na Alexandre Lacazette wote wametemwa kwenye kikosi cha Ufaransa kuelekea Fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao.
    Kocha Didier Deschamps amewaingiza wachezaji wote hao kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba, kama itatokea kati ya aliowateua watapata tatizo atawageukia Martial na Lacazette.
    Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud amebahatika kuingia kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji 23 pamoja na Kylian Mbappe, Ousmane Dembele, Nabil Fekir, Thomas Lemar, Antoine Griezmann na Florian Thauvin.

    Kikosi kamili cha Ufaransa cha Kombe la Dunia katika picha iliyothibitishwa kwenye Twitter jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    KIKOSI KAMILI CHA UFARANSA KOMBE LA DUNIA 

    Makipa: Areola, Lloris, Mandanda
    Mabeki: Hernandez, Kimpembe, Mendy, Pavard, Rami, Sidibe, Umtiti, Varane.
    Viungo: Kante, Matuidi, N'Zonzi, Pogba, Tolisso
    Washambuliaji: O. Dembele, Fekir, Giroud, Griezmann, Lemar, Mbappe, Thauvin.

    WACHEZAJI WA AKIBA

    Ben Yedder, Coman, Costil, Debuchy, Digne, Lacazette, Martial, Rabiot, Sakho, Sissoko, Zouma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LACAZETTE NA MARTIAL WOTE NJE KIKOSI CHA UFARANSA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top