• HABARI MPYA

  Friday, May 18, 2018

  YANGA SC WAIFUATA MWADUI FC KWA BASI MECHI JUMAPILI KAMBARAGE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka mjini Dar es Salaam Alfajiri ya leo kwa basi lake kwenda Shinyanga tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga Jumapili.
  Wachezaji 20 na  viongozi wanane wapo kwenye msafara huo unaotarajiwa kuwasili Shinyanga leo jioni tayari kwa mchezo huo wa Ligi Kuu.
  Yanga SC inahitaji kushinda mechi zake zote nne zilizobaki ili kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu, dhidi ya wapinzani wao katika kinyang’anyiro cha nafasi hiyo, Azam FC.

  Azam FC waliobakiza mechi mbili, wana pointi 52 katika nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa Simba SC webnye pointi 68 za mechi 28 kati ya 30, wakati Yanga SC yenye pointi 48 ni ya tatu.  
  Ligi Kuu inaendelea leo kwa mechi moja, Stand United wakiwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Na kesho kutakuwa na mechi mbili, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Simba SC wataikaribisha Kagera Sugar na Njombe Mji FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja Saba Saba mjini Njombe.
  Jumapili mbaki na Yanga SC kumenyana na Mwadui FC, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam, wenyeji Azam FC wataikaribisha Tanzania Prisons.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAIFUATA MWADUI FC KWA BASI MECHI JUMAPILI KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top