• HABARI MPYA

  Thursday, May 17, 2018

  BANDA ATINGA OFISINI KWA BALOZI NCHINI AFRIKA KUSINI NA KUMPA JEZI YA BAROKA FC

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kimataifa nchini, Abdi Hassan Banda jana alimtembelea Balozi wa Tanzania wa Afrika Kusini, Sylvester Ambokile Mwakinyule na kumkabidhi zawadi ya jezi ya klabu yake, Baroka FC.
  Mchezaji huyo wa Baroka FC ya Afrika Kusini ametumia muda wake wa mapumziko kabla ya kurejea nyumbani kwa kumtembelea Balozi Ambokile ofisini kwake mjini Pretoria.
  “Nimepata bahati ya kumtembelea Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mheshimiwa Ambokile na kumpa zawadi hii,”ameposti Banda katika ukurasa wake wa Instagram.
  Banda amekamilisha msimu wake wa kwanza Baroka FC tangu asajiliwe kutoka Simba SC ya Dar es Salaam, alikocheza kwa misimu mitatu baada ya kuwasili akitokea Coastal Union ya kwao mkoani Tanga.
  Abdi Banda (kulia) akimkabidhi jezi ya Baroka FC Balozi wa Tanzania wa Afrika Kusini, Sylvester Ambokile jana 

  Abdi Banda katika picha ya pamoja na Baroka FC Balozi Sylvester Ambokile jana mjini Pretoria  

  Hata hivyo, mume huyo mtarajiwa wa Zabib Kiba, dada wa mwanamuziki Ali KIba hakuwa na msimu mzuri sana wa kwanza Baroka FC, kwani timu hiyo imenusurika kushuka daraja.
  Banda ataendelea kucheza Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini msimu ujao pamoja na timu yake, Baroka FC kuchapwa bao 1-0 na SuperSport United katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe mjini Pretoria wiki mbili zilizopita.
  Baroka imekuwa timu ya mwisho baada ya timu mbili, Platinum Stars na Ajax Cape Town kuteremka, ikiwa imejikusanyia pointi 34 katika mechi 30.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BANDA ATINGA OFISINI KWA BALOZI NCHINI AFRIKA KUSINI NA KUMPA JEZI YA BAROKA FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top