• HABARI MPYA

  Friday, May 11, 2018

  AMMY NINJE AAHIDI USHINDI NGORONGORO HEROES DHIDI YA MALI JUMAPILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes Ammy Ninje ameahidi ushindi katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) mwakani Niger.
  Ninje amesema Mali ni timu nzuri ambayo amekuwa akiifuatilia kwa karibu, lakini kwa upande wao wamekuwa katika maandalizi ya kuhakikisha wanafanya vizuri na wachezaji wanaonekana kuyashika vyema mafunzo yake.
  Amesema hata kambi ya kikosi hicho imekuwa na morali kubwa yenye kiu ya kutaka kufanya vizuri na kufuzu kwenda raundi ya Tatu ambayo ndio ya mwisho kabla ya kufuzu kucheza fainali hizo za Africa kwa vijana.
  Amewataka waTanzania kujitokeza kwa wingi Jumapili ili kuwaongezea nguvu zaidi  vijana hao ya kufanya kile ambacho wa Tanzania wengi wangependa kukiona.
  Naye Issa Makamba, Nahodha wa kikosi hicho amesema wachezaji wako tayari kwa mapambano ambayo wanaamini watashinda.
  Mali, The Eagles waliwasili Dar es Salaam jana asubuhi kwa mafungu mawili, la kwanza likiwa na watu tisa na la pili likiwa na watu 20 na wamefikia katika hoteli ya Millennium Tower, Kijitonyama.
  Marefa kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani wamewasili leo pamoja na Kamisaa kutoka Shelisheli na viingilio katika mchezo huo vitakuwa Sh. 3,000 kwa VIP zote na Sh. 1, 000 kwa mzunguko wote.
  Wakati Ngorongoro hawajawahi kucheza fainali za AFCON U20, mafanikio makubwa ya Mali ni kushika nafasi  ya tatu katika Kombe la Dunia la FIFA la U20 mwaka 1999, baada ya kuifunga Senegal katika mchezo wa kuwania Medali ya Shaba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMMY NINJE AAHIDI USHINDI NGORONGORO HEROES DHIDI YA MALI JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top