• HABARI MPYA

  Saturday, May 12, 2018

  ABDI BANDA APAMBANA LEO AFRIKA KUSINI KUBAKI LIGI KUU

  Na Mwadishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za SuperSport United na Baroka FC zinatarjiwa kumenyana leo katika mchezo wa  kuwania kubaki Ligi Kuu ya Absa Afrika Kusini Uwanja wa Lucas Moripe Saa 10:00 jioni ya eo.
  Timu zote zipo katika nafasi mbaya na ni ushindi tu utakazozibakisha Ligi Kuu kwenye mechi hiyo ya mwisho.
  SuperSport wanashika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 33, pointi mbili zadi ya Ajax Cape Town wanaoshika nafasi ya 15, ambao wanamenyana na Kaizer Chiefs wikiendi hii.
  Baroka inashika nafasi ya 12 kwa pointi zake 34, pointi moja zaidi ya Polokwane City iliyopo nafasi ya 13 na pointi moja zaidi ya wapinzani wao wa leo.

  Abdi Banda kwa sasa anapamnama tmu yake isisuke Daraja Afrika Kusini

  Sare inaweza kuziepusha timu zote kushuka Daraja, lakini itategemea na matokeo ya Ajax, kama wataifunga Chiefs, watapaa juu ya SuperSport na Baroka.

  Vikosi vinatarajiwa kuwa: SuperSport: Williams, Kekana, Gould, Daniels, Bhasera, Furman, Mokoena (Letsholonyane 85’), Phala (Nhlapo 77’), Modiba, Mnyamane, Rusike.
  Baroka;: Vries, Motupa, Nguzana (Ngalande 62’), Mothupa, Kgoetyane, Banda, Mosele, Moet (Kgaswane 68’), Mabotja, Chawapiwa, Mdatsane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ABDI BANDA APAMBANA LEO AFRIKA KUSINI KUBAKI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top