• HABARI MPYA

    Saturday, May 12, 2018

    NONGA NA MSEMO WAONDOLEWA KWENYE LIGI KWA SABABU...

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro.
    Taarifa ya Ofisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo imesema kwamba  waamuzi walioondolewa katika orodha hiyo ni Seleman Nonga kutoka Arusha aliyekuwa katika kituo cha Geita na Dadu Fadhil Msemo wa Kilimanjaro aliyekuwa kituo cha Singida.
    Ndimbo amesema kwamba Nonga ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji, kushindwa kumudu mchezo, kukosa umakini, kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba A7 kati ya Kumuyange FC dhidi ya Ambassador.

    Wallace Karia, Rais wa TFF imewaondoa waamuzi wawili kwenye Ligi ya Mabingwa wa Mikoa  

    Kuhusu Msemo, Ndimbo amesema ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba C6 kati ya Temeke Squad dhidi ya Mtwivila City.
    Ndimbo amesema waamuzi hao wawili wanatakiwa kuondoka kwenye vituo vya Geita na Singida leo Jumamosi Mei 12,2018.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NONGA NA MSEMO WAONDOLEWA KWENYE LIGI KWA SABABU... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top