• HABARI MPYA

  Saturday, June 08, 2019

  SIMBA SC WAJITOA KOMBE LA KAGAME, WATANI WAO YANGA SC NAO WASEMA WANAJIFIKIRIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wametangaza kujiondoa rasmi kwenye michuano ya Klabu Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Julai mwaka huu nchini Rwanda. .
  Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema sababu za uamuzi huo ni muda wa maandalizi ya msimu ujao kuwa finyu kwani kuna baadhi ya wachezaji wao wako kwenye AFCON na watakaporejea hawatakuwa na muda wa kutosha wa kuwa pamoja.
  Amesema mpango wao ni kuweka kambi ya muda usiopungua wiki sita nje ya nchi wakiwa na dhamira ya kufanya vizuri zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo ratiba ya Kagame itaingiliana na ratiba ya kambi hiyo.

  "Tumepanga kufanya pre-season ya wiki sita kwakuwa tuna lengo la kufanya vizuri zaidi msimu ujao kwenye mashindano ya Kimataifa", amesema Magori na kuweka bayana kuwa tayari wameshaiandikia barua TFF juu ya uamuzi huo.
  Wakati Simba wakiyatosa mashindano hayo, uongozi wa Yanga umethibitisha kupokea barua ya mwaliko wa kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutoka CECAFA.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omar Kaya amesema bado wanatafakari na kufanya tathmini kuona ni faida gani watazipata kabla ya kutoa jibu la mwisho. 
  Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Azam FC ndiyo timu pekee kutoka Tanzania ambayo imekwishathibitisha kushiriki na imepanga kuanza mazoezi yake rasmi Juni 20 kabla ya kuondoka nchini Julai 4, 2019, kuelekea Kigali Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAJITOA KOMBE LA KAGAME, WATANI WAO YANGA SC NAO WASEMA WANAJIFIKIRIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top