• HABARI MPYA

  Wednesday, June 12, 2019

  TFF YAACHANA NA MKURUGENZI WAKE WA UFUNDI, AMMY NINJE NA MAKOCHA WOTE WA SERENGETI BOYS

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeachana na Mkurugenzi wake wa Ufundi, Ammy Conrad Ninje pamoja na kuvunja benchi zima la ufundi la timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
  Hatua hiyo inakuja baada ya Serengeti Boys kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U17) chini ya Kocha Mkuu, Oscar Milambo Aprili mwaka huu mjini Dar es Salaam.
  Pamoja na kuwa wenyeji, Tanzania ilitolewa kwenye AFCON U17 kinyonge baada ya kupoteza mechi zote tatu, ikifungwa 4-2 na Angola, 3-0 na Uganda na 5-4 na Nigeria mechi zote ikicheza Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

  Ammy Ninje ameachia Ukurugenzi wa Ufundi wa TFF kwa sababu za kifamilia 

  Na kuhusu Ninje, Rais wa TFF, Wallace Karia mchezaji huyo wa zamani wa Taifa Stars amemua kuacha kazi kwa sababu za kifamilia.
  Awali ya hapi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwataka Watanzania kununua jezi za timu ya taifa, Taifa Stars kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baadaye mwezi huu nchini Misri.
  Makonda ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za Taifa Stars na timu zote za taifa kwa ujumla nchini leo mjini Dar es Salaam.
  Makonda alisema kila Mtanzania anapaswa kuunga mkono ununuzi wa jezi hizo ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo wachezaji wa Taifa Stars wakati wa AFCON.
  Alisema jezi hizo zitakazoanza kutumika kesho kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri mjini Alexandria ni kielelezo cha nchi kutokana na rangi zake. “Itapendeza kila Mtanzania akiwa na jezi hizi na kuvaa wakati timu zetu zikiwakilisha nchi yetu katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,” amesema Makonda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAACHANA NA MKURUGENZI WAKE WA UFUNDI, AMMY NINJE NA MAKOCHA WOTE WA SERENGETI BOYS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top