• HABARI MPYA

  Monday, June 17, 2019

  WAZIRI DK. MWAKYEMBE AWAMAHASISHA WANANCHI KUICHANGIA TAIFA STARS AFCON

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka Watanzania kuchangia timu yao ya taifa ya soka, Taifa Stars inayojiandaa kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).        
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Waziri Mwakyembe amesema ni jukumu la kila Mtanzania kuchangia kiasi chochote kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wachezaji.
  Alisema kuwa kuna baadhi ya nchi zimetangaza kutoa magari na vitu mbalimbali nao wameamua kuanzisha kitu ambacho kitawapa morali vijana wao.

  Alisema kuna akaunti mbili maalum ambazo zitakuwa zikiingizwa fedha hizo, ambazo ni CRDB no 01J109956700 na ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) 0111010009781 pamoja namba ya simu ya mkononi 0735414043 ya Oscar Zabron.                     
  Alisema siku ya Alhamisi watakuwa na hafla ya maalum ambayo itakuwa ya moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na kuandaa vyeti maalum vya shukurani kwa watakaochangia.                     
  "Watanzania sio lazima uwe na uwezo kiasi chochote kile hata 2,500 inapokelewa na kuwepo sehemu ya zawadi kwa wachezaji wetu" alisema Mwakyembe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI DK. MWAKYEMBE AWAMAHASISHA WANANCHI KUICHANGIA TAIFA STARS AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top