• HABARI MPYA

  Saturday, June 15, 2019

  KAMA WEWE NI YANGA KWELI HUWEZI KUKOSA “KUBWA KULIKO” DIAMOND JUBILEE LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Hamasa na uchangishaji ya Yanga SC imesema maandalizi ya kuelekea kwenye tukio la #KubwaKuliko linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee yamekamiliaka.
  Katibu wa kamati hiyo Deo Mutta amesema tukio hilo litaanza saa 4:00 asubuhi na litarushwa LIVE na Televisheni ya Azam kupitia chaneli ya Azam Sports 2.
  Mutta amesema kwamba mgeni rasmi katika tukio hilo atakuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

  Mutta amesema pamoja na JK, watakuweoi viongozi wengine wakubwa wa nchi wakiongozwana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
  “Tunatarajia kuwa na tuko la kipekee hapo kesho kuanzia saa 4 asubuhi ndani ya Diamond Jubilee. Kumbuka unaweza kupata tiketi yako kwa shilingi 20,000 (elfu 20) tu, hakikisha una tiketi yako leo,”amesema Mutta.
  Mutta amesema katika tamasha hilo la kihistoria, Wasanii mbalimbali nyota watakuwepo kwenye tamasha hilo, wakiweko waigizaji na wanamuziki pia.
  Na tiketi zinaendelea kuuzwa kwenye vituo vya  Clouds Media (Mikocheni), EFM (Kawe), Born To Shine (Mwenge), Mr Price (Mlimani City), Big Respect (Kariakoo), Flamingo Pharmacy (Tabata) na Vunja Bei (Sinza).
  Vituo vingine ni Dar Live (Mbagala) Fettylicius (City Mall), Dick Sound (Magomeni), Total Azikiwe Station (Posta Mpya), Kings Barber Shop (Kigamboni), Robby One Fashion (Kinondoni) na makao makuu ya klabuni makutano ya mitaa ya twiga na Jangwani
  Lengo la tamasha hilo ni kuchangisha fedha za kufanyia usajili wa klabu ili waweze kushindana na mahaismu wao, Simba SC wanaojivunia uwekezaji wa bilionea, Mohammed ‘Mo’ Dewji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMA WEWE NI YANGA KWELI HUWEZI KUKOSA “KUBWA KULIKO” DIAMOND JUBILEE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top