• HABARI MPYA

  Thursday, June 27, 2019

  ALGERIA YATANGULIA 16 BORA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA

  BAO pekee Mohamed Youcef Belaili limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Algeria dhidi ya Senegal katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 leo Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo, Misri.
  Mshambuliaji huyo wa Esperance ya kwao, alifunga bao hilo dakika ya 49 akimalizia kazi nzuri ya kiungo wa Galatasaray ya Uturuki, Sofiane Feghouli.
  Matokeo hayo yanaihakikishia tiketi ya hatua ya 16 Bora Algeria wakifikisha pointi sita kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Kenya kwenye mchezo wa kwanza wa kunzi hilo.
  Sasa Senegal watakuwa na wajibu wa kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Kenya ili kwenda hatua ya mtoano.

  Mchezo mwingine wa kundi hilo unafuatia Saa 5:00 usiku kati ya Kenya na Tanzania, wapinzani wa Afrika Mashariki wanaozungumza lugha moja, Kiswahili na majirani kweli.
  Mapema jioni ulitangulia mchezo wa Kundi B na bao pekee la kiungo wa Sporting Charleroi ya Ubelgiji, Marco Ilaimaharitra dakika ya 76 likatosha kuipa Madagascar ushindi wa 1-0 dhidi  Burundi Uwanja wa Alexandria Alexandria.
  Msimamo wa Kundi B sasa Nigeria inaongoza kwa pointi zake sita na imekwishafuzu 16 Bora, ikifuatiwa na Madagascar yenye pinti nne, Madagascar yenye pointi moja na Burundi haina kitu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALGERIA YATANGULIA 16 BORA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top