• HABARI MPYA

  Sunday, June 30, 2019

  CAMEROON YAJIWEKA NJIA PANDA KUFUZU 16 BORA AFCON

  MABINGWA watetezi, Cameroon wamelazimishwa sare ya 0-0 na Ghana katika mchezo mkali wa Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 usiku wa jana Uwanja wa Ismailia.  
  Matokeo hayo japo yanaifanya Cameroon iendelee kuongoza kundi hilo kwa pointi zake nne baada ya kucheza mechi mbili, lakini hayaihakikishii nafasi ya kwenda 16 Bora.
  Kwani baada ya mchezo kati ya Benin na Guinea-Bissau kumalizika kwa sare ya 0-0 pia, kila timu katika kundio hilo ina nafasi ya kwenda hatua ya 16 Bora kama itashinda mechi yake ya mwisho.

  Mkongwe wa Ghana, Asamoah Gyan akijaribu kumtoka kiungo wa Cameroon, Michael Ngadeu-Ngadjui jana 

  Ghana inafuatia ikiwa na pointi mbili sawa na Benin, wakati hata Guinea-Bissau yenye pointi moja ikishinda mechi yake ya mwisho inaweza kusonga mbele kama wapinzani watapoteza.
  Cameroon nayo itahitaji japo sare kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Benin Julai 2 ili kujihakikishia tiketi ya hatua ya mtoano.  
  Mchezo mwingine wa Kundi E jana jioni baina ya Mauritania na Angola ulimalizika kwa sare ya 0-0 pia na maana yake kundi hilo nalo linakuwa na hadithi sawa na Kundi F – timu yoyote inaweza kufuzu hatua ya 16 Bora.
  Mali inaongoza ikiwa na pointi nne ikifuatiwa na Tunisa na Angola zenye pointi mbili kila moja, wakati Mauritania yenye pointi moja inashika mkia.
  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi nne; Kundi B Madagascar na Nigeria, Burundi na Guinea zote zitaanza Saa 1:00 usiku na za Kundi A Uganda na wenyeji, Misri na Zimbabwe dhidi ya DRC zote zikianza 4:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YAJIWEKA NJIA PANDA KUFUZU 16 BORA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top