• HABARI MPYA

  Wednesday, June 19, 2019

  SIMBA SC YALETA BEKI WA KATI MBRAZIL KUTOKA INDIA NA MSHAMBULIAJI WA KAIZER CHIEFS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba SC iko mbioni kuwasajili wachezaji wawili wa kigeni, beki wa kati Mbrazil, Gerson Fraga Vieira maarufu tu kama Gerson na mshambuliaji Ryan Moon kutoka Afrika Kusini.
  Gerson anatokea klabu ya ATK ya India na Moon anatokea Kaizer Chiefs ya kwao, Afrika Kusini na wote wanakuja kujaribu kusajiliwa Simba SC baada ya kumaliza mikataba na klabu zao na kuruhusiwa.
  Gerson Fraga Vieira mwenye umri wa miaka 26, mzaliwa wa Porto Alegre nchini Brazil, kisoka aliibukia timu ya vijana ya Gremio mwaka 2000 ambayo aliichezea hadi mwaka 2012 alipopandishwa timu ya wakubwa na akadumu hadi 2016.
  Beki wa kati Mbrazil, Gerson Fraga Vieira anakuja SImba SC kutoka  ATK ya India  
  Mshambuliaji Ryan Moon anakuja Simba SC kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

  Lakini sababu mbalimbali, akiwa Gremio alitiolewa kwa mkopo timu mbalimbali zikiwemo Oeste (2012), Red Bull Brasil (2014), Atenas (2014–2015), Red Bull Brasil (2015–2016) kabla ya kuuzwa moja kwa moja Mumbai City ya India mwaka 2016.
  Mwaka 2017 alihamia Atletico Tubarao alikocheza mechi 14 na kufunga bao moja kabla ya kurejea Mumbai City alikocheza hadi mwaka jana akahamia Renofa Yamaguchi ambako baada ya muda mfupi, akaondoka pia.
  Vieira ambaye pia Amechezea pia timu za taifa za vijana za Brazil chini ya umri wa mkiaka 15 (U15) na U17, Renofa Yamaguchi alicheza mechi nne tu akahamia ATK alikocheza mechi 13 na kufunga bao moja pia kabla ya kuja kujaribu bahati yake Simba.
  Kwa upande wake, Moon mwenye umri wa miaka 22, mzaliwa wa Pietermaritzburg, KwaZulu-Natal, Afrika Kusini baada ya kufanya vizuri na timu ya Maritzburg United aliyojiunga nayo akitoka kuzichezea Woodlands FC na Pirates FC, alipandishwa timu ya wakubwa mwaka 2016.
  Baada ya hapo alihamia Kaizer Chiefs mwaka 2016 ambako alidumu hadi mwishoni mwa msimu alipoachwa na sasa anakuja kujaribu bahati yake Simba SC.
  Amewahi pia kuchezea timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ kuanzia mwaka 2017 kwa mechi nane na kufunga bao moja tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YALETA BEKI WA KATI MBRAZIL KUTOKA INDIA NA MSHAMBULIAJI WA KAIZER CHIEFS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top