• HABARI MPYA

  Friday, June 21, 2019

  SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI KUTOKA TIMU YA LIGI DARAJA LA NNE NCHINI BRAZIL

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mbrazil, Wilker Henrique da Silva amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu bingwa ya Tanzania Bara, Simba SC.
  Silva mwenye umri wa miaka 23 tu ametambulishwa leo na Mwenyekiti wa klabu, Swedi Nkwabi na anajiunga na Simba SC akitokea klabu ya Bragantino inayocheza Ligi Daraja la Nne nchini Brazil.
  Silva anakuwa mchezaji wa nne rasmi kusajiliwa Simba SC baada ya baada ya kipa Beno Kakolanya kutoka Yanga, beki wa kati, Kennedy Wilson Juma kutoka Singida United wote Watanzania na kiungo wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman.
  Mshambuliaji Mbrazil Wilker da Silva (kulia) akiswaini mkataba wa kujiunga na Simba SC pembeni ya Mwenyekiti wa klabu, Swedi Nkwabi


  Silva amekuwa mchezaji wa Bragantino tangu mwaka 2015 alipojiunga nayo kutoka Ponte Preta, ingawa mwaka 2018 alikwenda kuichezea Uniao Barbarense iliyokuwa Daraja la tatu kabla ya kurejea timu yake hiyo hadi sasa anatua Msimbazi.
  Taarifa zaidi zinasema kwamba Simba SC ipo kwenye mazungumzo na mawakala wa wachezaji kadhaa na wengine imeripotiwa wapo njiani nchini.
  Miongoni mwao ni beki wa kati Mbrazil, Gerson Fraga Vieira kutoka ATK ya India na mshambuliaji Ryan Moon kutoka Kaizer Chiefs ya kwao, Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI KUTOKA TIMU YA LIGI DARAJA LA NNE NCHINI BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top