• HABARI MPYA

  Friday, June 21, 2019

  HASSAN KESSY ARUHUSIWA KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA SIMBA WA TERENGA JUMAPILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limemruhusu beki wa Tanzania, Hassan Ramadhani Kessy kuichezea timu yake ya taifa katika mchezo wa kwanza wa Kundi C Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Senegal Jumapili.
  Hiyo ni baada ya CAF kujiridhisha kwamba beki huyo wa kulia wa Nkana FC ya Zambia hana kadi mbili za njano kama ilivyofikiriwa na sasa yuko huru kuwavaa Simba wa Teranga keshokutwa.
  Awali ilisemekana Kessy, mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Simba na Yanga za nyumbani, Tanzania alikuwa ana kadi anatumikia adhabu ya kazi ambazo zingemfanya asicheze mchezo huo – lakini imeelzwa alimaliza adhabu katika mchezo namba 101 dhidi ya Cape Verde kufuzu AFCON.

  Hassan Kessy ameruhusiwa kuichezea Taifa Stars dhidi ya Senegal Jumapili 

  AFCON 2019 inaanza leo nchini Misri, kwa wenyeji, Mafarao kuumana na Zimbabwe kuanzia Saa 11:00 jioni Uwanja wa Kimataifa wa Cairo katika mchezo wa Kundi A.
  Kesho kutakuwa na mechi mbili, ya Kundi A Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikimenyana na Uganda kuanzia Saa 11:30 itakayofuatiwa na za Kundi B Nigeria dhidi ya Burundi Saa 2:00 usiku na Guinea na Madagascar Saa 5:00 usiku.
  Taifa Stars itatupa kete yake ya kwanza jumapili kwa kumenyana na Simba wa Teranga kuanzia Saa 2:00 usiku, itakayofuatiwa na mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Algeria na Kenya Saa 5:00 usiku, ambazo zitatanguliwa na mechi ya Kundi D kati ya Morocco na Namibia Saa 11:30 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HASSAN KESSY ARUHUSIWA KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA SIMBA WA TERENGA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top