• HABARI MPYA

  Friday, June 21, 2019

  SIMBA SC YAIPIGA GWAMBINA FC KWA MATUTA BAADA YA SARE YA 1-1 MISUNGWI LEO

  Na Mwandishi Wetu, MISUNGWI
  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 na Gwambina FC katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Gwambina huko Misungwi mkoani Mwanza.
  Gwambina walitangulia kwa bao la mapema la Anwar Jabir kabla ya kiungo na Nahodha wa Simba leo, Said Hamisi Ndemla kuisawazishia timu yake dakika tano kuelekea filimbi ya mwisho.
  Na katika mikwaju ya penalti mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mara mbili mfululizo hawakufanya makosa, wakailaza Gwambina 4-2 katika uzinduzi wa Uwanja wa timu hiyo. 

  Said Ndemla aliisawazishia Simba SC kabla ya kuibuka na ushindi wa penalti 4-2

  Gwambina iliyokuwa Ligi Daraja la Tatu, itashiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara msimu ujao, baada ya kuinunua timu ya Arusha United. 
  Na katika kujiandaa na msimu ujao baada ya kufanikisha ujenzi wa Uwanja wake wa kisasa, Gwambina imecheza na mabingwa wa nchi leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIPIGA GWAMBINA FC KWA MATUTA BAADA YA SARE YA 1-1 MISUNGWI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top