• HABARI MPYA

  Sunday, June 16, 2019

  RAIS KIKWETE AWAASA VIONGOZI KUTOTUMIA USHABIKI KUKANDAMIZA TIMU NYINGINE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete amewaasa viongozi nchini kutotumia ushabiki wao wa mpira kukandamiza timu pinzani.
  Jakaya, maarufu kama JK ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye tamasha maalum la kuchangia klabu ya Yanga Jumamosi ukumbi wa Diamond Jubilee lililojulikana kama “Kubwa Kuliko”.
  “Unatumia ushabiki wako wa mpira kukandamiza timu nyingine,” alisema Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitoa angalizo kwa viongozi wa Serikali.

  Pamoja na hayo, Rais Kikwete klabu nchini ziwekeze kwenye soka ya vijana ili kuinua vipaji kuliko kugombea wachezaji wa kigeni, kwani kufanya hivyo ni kuawafaidishia wenzao.
  Rais Mstaafu Kikwete pia alisema Yanga kwa sasa imepoteza makali yake kiasi kwamba inazidiwa na mahasimu wao wa jadi, Simba.
  Kauli hiyo iliungwa mkono na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alisema klabu hiyo inatakiwa kujiimarisha tena ili kurejesha ushindani katika soka nchini; “Bila Yanga imara, hakuna Simba imara,” alisema Majaliwa.
  Pamoja na hayo, Waziri Mkuu alitoa Sh. Milioni 10 kama mchango wake kwenye harambee ya Yanga, huku Kikwete akichangia Sh. Milkioni 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS KIKWETE AWAASA VIONGOZI KUTOTUMIA USHABIKI KUKANDAMIZA TIMU NYINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top