• HABARI MPYA

  Friday, June 14, 2019

  SULEIMAN MATOLA AACHANA NA LIPULI FC, AJIUNGA NA TIMU YA POLISI TANZANIA

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Polisi Tanzania ya Kilimanjaro itakayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao imemtambulisha rasmi Selemani Matola kuwa kocha wake msaidizi.
  Matola ambaye ni kiungo wa zamani wa Simba, alikuwa kocha msaidizi wa Lipuli FC kwa misimu miwili iliyopita akiiwezesha kumaliza nafasi ya sita na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) msimu uliopita.
  Polisi imepanda Ligi Kuu baada ya kuongoza Kundi B ikiungana na Namungo FC ya Lindi iliyoongoza Kundi A zikichukua nafasi za African Lyon na Stand United zilizoshuka moja kwa moja kutoka Ligi Kuu.

  Selemani Matola ameachana na Lipuli FC na kujiunga na Polisi Tanzania kama kocha wake msaidizi pia

  Polisi ilipanda Ligi Kuu ikiwa chini ya Kocha Mbwana Makatta ambaye baada ya hapo ameondolewa na sasa timu hiyo itaendelea kutafuta kocha Mkuu mwingine atakayefanya kazi na Matola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SULEIMAN MATOLA AACHANA NA LIPULI FC, AJIUNGA NA TIMU YA POLISI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top