• HABARI MPYA

  Saturday, June 22, 2019

  YANGA SC YAMSAINISHA MIAKA MITATU KIUNGO WA ALLIANCE FC, MAPINDUZI BALAMA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO chupukizi Mtanzania, Mapinduzi Balama amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam kutoka Alliance FC ya Mwanza.
  Balama ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita ambao ulimalizika kwa Simba SC, kutwaa taji la pili mfululizo, huku watani wao, Yanga wakishika nafasi ya pili.
  Mapinduzi anakuwa mchezaji mpya wa 10 kusajiliwa Yanga SC na wa tatu tu mzawa baada ya beki Ally Ally kutoka KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam na kiungo wa ulinzi, Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar.

  Mapinduzi Balama amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Yanga SC

  Wengine saba wote ni wa kigeni, Sadney Urikhob kutoka Namibia, Lamine Moro kutoka Ghana), Juma Balinya kutoka Uganda, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana wote wa Rwanda, Mustapha Seleman kutoka Burundi na Maybin Kalengo kutoka Zambia.
  Yanga SC imedhamiria kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, baada ya misimu miwili ya kuzidiwa kete na mahasimu wao, Simba SC.
  Baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu mitatu mfululizo 2015, 2016 na 2017, Yanga SC wakapokonywa taji hilo na Simba SC 2018 ambao wamefanikiwa kulitetea 2018.
  Kwa ujumla msimu huu Yanga imedharimia kuja kivingine, ikianza na ‘Wiki ya Mwanachi’ ambayo kilele chake kitakuwa Julai 27 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam siku ambayo itacheza mechi ya kutambulisha kikosi chake kipya na kauli mbiu yake itakuwa ‘Funga kazi, Kusanya Kijiji’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMSAINISHA MIAKA MITATU KIUNGO WA ALLIANCE FC, MAPINDUZI BALAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top