• HABARI MPYA

  Monday, June 17, 2019

  SIMBA NA YANGA ZASHINDA MECHI ZA MWISHO NA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam Jumapili.
  Kwa matokeo hayo, Simba SC inamaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo nyuma watani wao wa jadi, Yanga ambao baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliotangulia wamemaliza kileleni.
  Msimamo wa kundi hili unaonyesha Yanga wako kileleni wakiwa na pointi saba, wakifuatiwa na Simba yenye pointi nne sawa na Kagera Sugar ambao wamezidiwa wastani wa mabao.

  Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Andrew Michael dakika ya saba na 20 na Modest Modest dakika ya 33 kwa penalti, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Abinus Kahatano dakika ya 79, wakati kwenye mchezo wa kwanza bao pekee la Yanga lilifungwa na Erick Msagati dakika ya 11.
  Kwa matokeo hayo Simba na Yanga wanatinga hatua ya nusu fainali na sasa wanasubiri kutambua wapinzani wao kutoka Kundi B ambao ni Azam FC na Mtibwa Sugar
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZASHINDA MECHI ZA MWISHO NA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI KUU YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top