• HABARI MPYA

  Wednesday, June 26, 2019

  CAMEROON YAANZA VYEMA AFCON, GHANA YALAZIMISHWA SARE

  CAMEROON imeanza vyema Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau jaa katika mchezo wa Kundi F Uwanja wa Ismailia nchini Misri.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao ya Simba Wasiofungika, beki wa Panionios ya Ugiriki, Banana Yaya dakika ya 66 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji wa Karl Brillant wa Villarreal ya Hispania na Stephane Bahoken dakika ya 69.
  Ushindi huo unaifanya Cameroon inayofundishwa na nyota wa zamani wa Uholanzi, Clarence Seedorf na  Patrick Kluivert ianzie kileleni mwa Kundi C kwa pointi zao tatu, baada ya Ghana kulazimishwa sare ya 2-2 na Benin.


  Mabao ya Ghana yalifungwa na washambuliaji pacha na ndugu wawili, Andre Ayew anayechezea Fenerbahce ya Uturuki dakika ya 69 na mdogo wake, Jordan Ayew anayechezea Crystal Palace dakika ya 42, wakati ya Benin yote yalifungwa na mshambuliaji wa Adana Demirspor ya Uturuki pia, Mickae Pote dakika ya pili na 63.
  Sasa msimamo wa Kundi F lenye timu za Magharibi tupu Cameroon inaongoza kwa pointi zake tatu ikifuatiwa na Ghana na Benin zenye pointi moja kila moja, wakati Guinea-Bissau inashika mkia ikiwa haina pointi.
  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi tatu, Nigeria na Guinea Saa 11:30 jioni Kundi B, Uganda na Zimbabwe Saa 2:00 usiku na wenyeji, Misri dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Saa 5:00 usiku, zote za Kundi A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YAANZA VYEMA AFCON, GHANA YALAZIMISHWA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top