• HABARI MPYA

  Saturday, June 08, 2019

  REAL YATHIBITISHA KUMSAJILI HAZARD KWA PAUNI MILIONI 130

  Real Madrid imethibitisha kumsajili Eden Hazard kwa dau la Pauni Milioni 130 akisaini mkataba wa miaka mitano 

  TAKWIMU ZA HAZARD AKIWA NA CHELSEA 

  Mechi alizocheza: 352
  Mabao aliyofunga: 110
  Pasi za mabao: 92
  Mataji aliyoshinda:  Ligi Kuu (2014-15, 2016-17), Kombe la FA (2017-18), Kombe la Ligi (2014-15), Europa League (2012-13, 2018-19)
  KLABU ya Real Madrid imethibitisha kumsajili Eden Hazard kwa dau la Pauni Milioni 130 akisaini mkataba wa miaka mitano na itamtambulisha baadaye akikamilisha vipimo vya afya.
  Hatimaye Chelsea imekubali kumuuza Mbelgiji huyo baada ya vigogo hao wa Hispania kukubali kulipa dau lililotakiwa na kocha Mfaransa, Zinedine Zidane amempata mchezaji ambaye amekuwa akimuhitaji sana Santiago Bernabeu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesaini mkataba mrefu na Real Madrid na ndiye atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi, kwani mshahara wake ni Pauni 400,000 kwa wiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL YATHIBITISHA KUMSAJILI HAZARD KWA PAUNI MILIONI 130 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top