• HABARI MPYA

  Sunday, June 16, 2019

  YANGA YASAJILI MFUNGAJI BORA WA LIGI KUU YA UGANDA SIMBA WALIKUWA WANAMTAKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga SC imemsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Balinya Juma kutoka Polisi FC ya kwao. 
  Mchezaji huyo aliyeibuka mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Uganda msimu uliopita akifunga mabao 17 ametambulishwa Jumamosi katika tamasha la Kubwa Kuliko lilifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Dar es Salaam.
  Baada ya kufanya vizuri msimu uliopita, Balinya aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Uganda Machi mwaka huu, lakini hakubahatika kuteuliwa kwenye kikosi kilichokwenda kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

  Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Balinya Juma ametua Yanga kutoka Polisi FC ya kwao 

  Sambamba na mchezaji huyo ambaye imeripotiwa mahaismu wao, SImba SC pia walikuwa kwenye harakati za kumsajili, Yanga pia imemtambulisha rasmi leo kiungo wa ulinzi, Abdulaziz  Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASAJILI MFUNGAJI BORA WA LIGI KUU YA UGANDA SIMBA WALIKUWA WANAMTAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top