• HABARI MPYA

  Wednesday, June 26, 2019

  MAYANJA ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUJIUNGA NA KMC YA KINONDONI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEWAHI kuwa Kocha wa Simba SC, Mganda Jackson Mayanja leo ametambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa klabu ya KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam.
  Mayanja amejiunga KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja aliousaini leo baada ya kuwasili nchini mbele ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta.
  “Ni kocha mwenye uzoefu wa ligi ya Tanzania hadi katika mashindano ya kimataifa, anaanza rasmi kazi ya kuinoa KMC inayojiandaa na mashindano ya Kagame Cup na Kombe la Shirikisho barani Afrika,”imesema taarifa ya KMC leo.
  Pamoja na Simba SC, Mayanja pia amewahi kuzifundisha timu za Kagera Sugar ya Bukoba na Coastal Union ya Tanga kwa hapa Tanzania.

  Jackson Mayanja (kulia) leo baada ya kutambulishwa kuwa kocha mpya wa klabu ya KMC  

  Kwa Uganda, baada ya kuwa kiungo tegemeo wa timu ya taifa, The Cranes miaka ya 1980 hadi 1990 mwanzoni, Mayanga pia alizichezea kwa mafanikio klabu za KCCA, Kampala ya kwao na El- Masry ya Misri.
  KMC imemchukua baada ya kumpoteza kocha wake, Mnyarwanda, Mrundi Ettienne Ndayiragijje aliyechukuliwa na klabu ya Azam FC ya nyumbani.
  Mtihani wa kwanza wa Mayanja KMC itakuwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mwezi ujao nchini Rwand.
  Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kati ya Agosti na Septemba, lakini mwishoni mwa mwaka itaanza kampeni za Kombe la Shirikisho Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYANJA ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUJIUNGA NA KMC YA KINONDONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top