• HABARI MPYA

  Wednesday, June 26, 2019

  KOTEI ASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU KUJIUNGA NA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mghana, James Agyekum amejiunga na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini baada ya kusiani mkataba wa miaka mitatu.
  Kaizer Chiefs imetambulisha rasmi Kotei leo mchana na ikisema kwamba imemsainisha mkataba wa miaka mitatu.
  Naye Kote hakuchukua muda mrefu kuposti kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwaaga rasmi Simba mashabiki wa Simba SC.
  “Kwa wapendwa mashabiki wangu wa Simba. Siku ya kwanza naiona ardhi ya nchi hii niliipenda na siku ya kwanza navaa jezi ya Simba nilijisikia furaha. Nilijivunia kuwa sehemu ya timu hii nzuri yenye mapenzi yasiyomithilika,”amesema Kotei.

  Lakini pia mchezaji huyo akaelezea kumbukumbu zake ikiwemo namna alivyoshinda taji la kwanza na Simba, Kombe la Azam Sports Federation Cup mwaka juzi mjini Dodoma na akatoa shukrani za pekee kwa mmoja wa vigogo wa klabu hiyo, Muslah Ruwaih.
  Mchezaji huyo ambaye Agosti 10 mwaka huu atafikisha umri wa miaka 26, alijiunga na Simba SC Desemba mwaka 2016 akitokea Al-Oruba ya Oman aliyoanza kuichezea mwaka 2015 akitokea Liberty Professionals ya kwao, Ghana iliyominua mwaka 2010.
  Kotei ambaye mwaka 2014 alicheza kwa mkopo BA Stars, alisajiliwa Simba pamoja na Mghana mwenzake, kipa Daniel Agyei aliyetokea Medeama SC ya kwao pia, lakini mlinda mlango huyo aliachwa baada ya msimu mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOTEI ASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU KUJIUNGA NA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top