• HABARI MPYA

  Thursday, June 20, 2019

  MAKONDA AWAPA TFF ENEO LA UKUBWA WA HEKARI 15 WAJENGE SHULE YA SOKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa eneo lenye ukubwa wa hekari 15 kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili wajenge shule ya mchezo huo na kambi ya timu ya taifa.
  Makonda ametoa ahadi hiyo leo katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuichangia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza kesho nchini Misri.
  “Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu kuwapatia Taifa Stars chini ya TFF eneo lenye ukubwa wa hekari 15 watakalojenga soccer technical school,” amesema Makonda.  Aidha, Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam alisema kwamba anashukuru anawapa eneo hilo TFF, wakati ambao imepokea fedha kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. 
  Makonda amewapa TFF eneo hilo akitoka kuipa klabu ya Yanga eneo la ukubwa wa hekari saba huko Kigamboni ili wajenge Uwanja.
  Na kwa sababu hiyo, Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara alimuomba Makonda aifikirie na klabu hiyo katika mgawo wake wa ardhi.
  “Binadamu tuna wivu…na siye tuna nyongo…ninakuomba Mkuu wa Mkoa...kufanya vizuri kote huko…robo fainali Klabu Bingwa Afrika…mbona haututaji katika neema hizi za ardhi…” alisema Manara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKONDA AWAPA TFF ENEO LA UKUBWA WA HEKARI 15 WAJENGE SHULE YA SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top