• HABARI MPYA

  Friday, June 21, 2019

  YANGA SC YAITANDIKA SIMBA 2-0 NA KUMALIZA NAFASI YA TATU LIGI YA VIJANA U20

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Yanga SC imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Simba SC.
  Ushindi huo wa Yanga SC umetokana na mabao ya wachezaji wake nyota, Kilaza Mazoea dakika ya 35 na Julius Wilson dakika ya 85 mchana wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam. 
  Wakati Yanga iliangukia kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu baada ya kufungwa na Azam kwa penalti 3-0 kufuatia sare ya 0-0, Simba SC ilichapwa 3-1 na Mtibwa Sugar katika mechi za Nusu Fainali hapo hapo Azam Complex. 

  Hicho kinakuwa kipigo pili Yanga U20 wanawapa watani wao wa jadi, Simba baada ya kipiga 2-1 kwenye mchezo wa Kundi A la michuano hii wiki iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAITANDIKA SIMBA 2-0 NA KUMALIZA NAFASI YA TATU LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top