• HABARI MPYA

  Saturday, June 15, 2019

  KUBWA KULIKO YAFANA; ROSTAM AZIZ AIPA YANGA SH MILIONI 200, GSM MILIONI 300 NA MAJALIWA…

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MFANYABIASHARA bilionea, Rostam Aziz ametoa kiasi cha Sh. Milioni 200 kuichangia klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam ifanikishe zoezi la usajili wa kuunda kikosi imara cha msimu ujao.
  Ofa hiyo ya Rostam, Mbunge wa zamani wa Igunga, Tabora na aliyekuwa kuwa Mweka Hazina wa CCM imetangazwa Jumamosi katika tamasha la Kubwa Kuliko lilifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Dar es Salaam.
  Pamoja na Rostazm, mfanyabiashara mwingine Ghalib kupitia kampuni yake ya GSM ameichangia klabu hiyo Sh. Milioni 300.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekuwa mgeni rasmi katika Kubwa Kuliko iliyotikisa mji Jumamosi hii ametoa Sh. Milioni 10.
  Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete aliyehudhuria pia shughuli hiyo kwa upande wake ametoa kiasi cha Sh. Milkioni 5.
  Mdhamini wa klabu ya Simba SC, Hamisi Kilomoni naye aliibukia kwenye Kubwa Kuliko na kuchangia Sh. 500,000.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga Anthony Mavunde amesema wamependekeza kwa uongozi kuanzisha wiki maalum itakayoitwa ‘Wiki ya Mwananchi’, itakakayokuwa maalum kwaajili ya wapenzi na wanachama wa Yanga kuitumikia jamii.
  Amesema wiki hiyo itakuwa ikifanyika mwezi Agosti kila mwaka na siku ya kilele chake kutafanyika tukio kubwa litakalofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam likiambatana na utambulisho wa wachezaji wao wapya.
  “Tumepanga tuwe na Wiki ya Mwananchi’, ambapo wanachama wa Yanga watafanya usafi maeneo katika hospitali, masoko na kutoa misaada mbalimbali. Wiki hiyo ikikamilika tutakutana Uwanja wa Taifa”, amesema Mavunde.
  Amesema wamemuomba Rais Magufuli na endapo ataridhia tukio hilo litafanyika mwaka huu ambapo miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni kutambulisha wachezaji wao wapya wanane ambao wamesajiliwa kutoka nje ya Tanzania kwaajili ya msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUBWA KULIKO YAFANA; ROSTAM AZIZ AIPA YANGA SH MILIONI 200, GSM MILIONI 300 NA MAJALIWA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top