• HABARI MPYA

  Friday, June 21, 2019

  MAKONDA AWAPA YANGA ENEO LENYE THAMANI YA SH MILIONI 700, TFF BILIONI 1.5

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amekabidhi maeneo ya ardhi kwa klabu ya Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) eneo la Kigamboni mjini humo kutimiza ahadi zake za hivi karibuni.
  Makonda amewapa Yanga eneo lenye ukubwa wa hekari saba pamoja na hati ya umiliki kwa klabu ya  Yanga kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na matumizi mengine, ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa hafla ya harambee ya uchangiaji wa timu hiyo Juni 5.
  Eneo hilo lenye thamani ya Shilingi Milioni 700 lipo umbali wa Kilomita 14 kutoka Daraja la Mwalimu Nyerere na umbali wa Mita 200 kutoka Barabara kubwa.
  Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo akiwakabidhi viongozi wa Baraza la Wadhamini wa Yanga nati za eneo lao leo 

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifuatilia maelekezo ya Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani kwenye makabidhiano leo 

  Pamoja na kuwapa Yanga eneo, Mkuu wa Mkoa, Makonda pia leo amekabidhi hekari 15 za ardhi kwa TFF zilizopo eneo la Kigamboni pia, Kisarawe 2 lenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 1.5.
  Wakati kwa Yanga SC, Makonda ametimiza ahadi ya Juni 5, TFF aliwapa ahadi hiyo jana hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuichangia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ziizoanza leo nchini Misri.
  Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara alimuomba Makonda aifikirie na klabu hiyo katika mgawo wake wa ardhi.
  “Binadamu tuna wivu…na siye tuna nyongo…ninakuomba Mkuu wa Mkoa...kufanya vizuri kote huko…robo fainali Klabu Bingwa Afrika…mbona haututaji katika neema hizi za ardhi…” alisema Manara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKONDA AWAPA YANGA ENEO LENYE THAMANI YA SH MILIONI 700, TFF BILIONI 1.5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top