• HABARI MPYA

  Thursday, June 20, 2019

  MKOA WA KIGOMA WATWAA UBINGWA WA MICHUANO YA KWANZA YA TAIFA YA U15

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Kigoma imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza wa taifa ya vijana chini ya umri wa miaka (U15) baada ya kuichapa Mjini Magharibi bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Bao pekee lililoipa ushindi Kigoma lilifungwa na mshambuliaji wake hodari, Hemed Hamisi  dakika ya 35 akitumia makosa ya beki wa Mjini Magharibi, Abdulrazak Vuai Mohamed aliyepiga fyongo katika jitihada za kuokoa na mpira ukamkuta mfungajii.
  Jumla ya timu 34 kutoka mikoa yote ya Tanzania zilishiriki michuano hiyo na Kigoma ambao kiasili ni mkoa wenye historia ya kutoa vipaji vingi imedhihirisha ubora wake kwa mara nyingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKOA WA KIGOMA WATWAA UBINGWA WA MICHUANO YA KWANZA YA TAIFA YA U15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top