• HABARI MPYA

  Sunday, June 23, 2019

  BRAZIL YAICHAPA PERU 5-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI COPA AMERICA

  Gabriel Jesus akiwa juu ya wachezaji wenzake wa Brazil wakati wa kushangilia ushindi wao wa 5-0 dhidi ya Peru kwenye mchezo wa Kundi A michuano ya Copa America Uwanja wa Arena Corinthians. Mabao ya Brazil yalifungwa na Casemiro dakika ya 12, Roberto Firmino dakika ya 19, Everton dakika ya 32, Dani Alves dakika ya 53 na Willian dakika ya 90, wakati Jesus alikosa penalti dakika ya 90 na ushei.
  Ushindi huo unaifanya Brazil itinge Robo Fainali baada ya kufikisha pointi saba katika mchezo wa tatu na wa mwisho hivyo kumalizia kileleni mwa Kundi A, ikifuatiwa na Venezuela pointi tano, Peru pointi nne wakati Bolivia imemaliza mkiani bila pointi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRAZIL YAICHAPA PERU 5-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI COPA AMERICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top